Kibaki, Raila, Uhuru, MaDVD, Kalonzo and Ruto In A Matatu

January 3, 2013
by

Conda: haya haya pesa kwa mkono…

Kibaki: wee kodaakta ni peesa gaapi, nashuuka haapo haapo beere…

Conda: finje…

Kibaki: mavi ya kuuku, buure kabisa! Hapaana, niko na forty, ama unifikiishe mpaka huuko huko kwa mraago diipo nikuupe iiyo fifty!

Conda: nyinyi wenye mnafinyana hapo nyuma-raila, uhuru na mudavadi, mtu akuje akae kwa hii nafasi ya mbele kibaki akishuka. Wee uhuru leta pesa yako…

Uhuru: nimekaa vibaya ntakupa huko mbele…..ama fanya hivi, mudavadi? si unilipie ntakurudishia kibaki akishuka nikikaa vizuri kwa iyo kiti yake?

Mudavadi: sawa nakulipia, lakini mimi ndio nakaa kwa iyo kiti kibaki anawacha sawa?

Uhuru: sawa basi…

Mudavadi: konda, chukua iyo soo kata ya wawili, mimi na uhuru…

Raila: omera ni mimi ndio nakaa kwa iyo kiti! Mimi ndio nimefinyana hapa kutoka mwanzo wa safari hadi hapa. Nyinyi mumepanda gari na karibu, hamjafinyana kwa muda murefu kama mimi!

Kibaki alights…

Uhuru: wee, mi ndio nakaa hapo!

Ruto: namsupport, uhuru akae hapo.

Mudavadi: wee uhuru, imekuwaje tena, si nafikiri tulikubaliana?

Uhuru: ziii, nilikuwa nakuenjoy bana, mashetani joh, madimoni nayo!

Mudavadi: sawa basi nkt! Wee konda, nirudishie finje yangu, huyu fala anajilipia!

Raila: deere, nimemalisa kuongea kwa simu. Sasa unaesa ongesa volume ya iyo ngoma-

‘kigeugeu eh eh! …..kigeugeu eh eh!’

Kalonzo: hi hii hiii sijui nichukue iyo kiti amaa, hapana, raila, maze chukua iyo kiti jooh, hawa viyana hawayui aney!

Kiyiapi: kwani mi ndio mnanionaje siezi kaa apo? Mi ndio niko na matako nusu nkt, mi ndio nakaa apo!
Courtesy 

Leave a Reply

Your email address will not be published.Don't Miss