Hamisa Asks for Forgiveness as She Turns Over a New Leaf

September 3, 2018

Hamisa Mobetto is on some ‘new month new me’ vibes.

As August came to a close and September dawned on us, the Tanzanian video vixen was self-reflective and she took to social media to pen a long statement about her apparent transformation and newfound growth.

In the statement, Hamisa, who has often made headlines for all the wrong reasons, acknowledged that the life she led before might have caused controversy, but she has since matured and learnt important life lessons.

“Dunia inaenda mbele na watu wanabadilika, pengine lifestyle ya zamani haikuwa nzuri na mpaka kusababisha ‘mambo flani flani’ kutokea katika maisha yangu lakini umri unapozidi kusonga mbele akili inatanuka na kujifunza mambo mengi kwenye maisha,” wrote Hamisa.

She went on to say: “Hamisa wa sasa sio kama yule wa zamani, nimezidi kuwa na akili yenye kupambanua mabaya na mazuri na kuchukua hatua ili kuenda na kasi ya ukuaji wa akili yangu.”

The mother of two also opened up about her baby daddies and thanked them for the support they have given her over time.

Hamisa further observed that she has previously been involved in online wrangles and apologised saying she is now looking for a fresh start.

Read her full statement below.

Pengine hufahamu alipotoka Hamisa Mobetto… Wacha nikufahamishe, nilianza kutambulika rasmi kwenye tasnia ya urembo mwaka 2010 baada ya kuibuka mshindi wa Miss XXL After School Bash. Njia ya mafanikio ilifunguka hapo na hatimae nilishiriki Miss Tanzania na Also Miss New World Tanzania Na Kua first Runner Up 2012.

Lakini Pia Nilifanikiwa Kushriki Miss UniAfrica na kuingia Top Ten… Safari ikaendelea na kwa kuwa urembo ni kipande cha sanaa niliingia kwa pia kwenye Bongo Movie na kucheza filamu kadhaa na huku pia nikiwa Video Vixen kwa baadhi ya nyimbo za Bongo Fleva… Nisieleweke vibaya kwa hili, kitanda hakizai haramu… nilipata mtoto wangu wa kwanza miaka michache iliyopita na ninashukuru katika mahusiano yale nilipendwa mimi na mwanangu na kuhudumiwa kwa kila kilichohitajika baadae tena nikapata mtoto mwengine katika mahusiano mengine ambayo pia yalikuwa mazuri na huduma zote kama kawaida zilikuwepo na zinaendelea kuwepo mpaka sasa… Shukrani kwa baba wote wa watoto wangu… Huyo ni mimi Hamisa Mobetto, safari hiyo imenifundisha mengi sana mpaka sasa na nafikiri nimekomaa kwa kiasi fulani… Nashukuru Hamisa Mobetto imekuwa Brand kubwa mpaka kufikia kunipa ‘Deals’ mbalimbali zinazoendelea kuja (Alhamdullilah).

Sio tu ‘Deals’ pekee bali hata fanbase imekuwa kubwa mno kitu ambacho ninakifurahia kwani ni Support kubwa sana ninaipata. Wapo walioamua kutengeneza page za Social Media mbalimbali kwa ajili ya kuonyesha support na wengine pia kutumia fursa hiyo kutengeneza ajira kupitia matangazo n.k nasemaje Yote Heri! 

Dunia inaenda mbele na watu wanabadilika, pengine lifestyle ya zamani haikuwa nzuri na mpaka kusababisha ‘mambo flani flani’ kutokea katika maisha yangu lakini umri unapozidi kusonga mbele akili inatanuka na kujifunza mambo mengi kwenye maisha. 
Hamisa wa sasa sio kama yule wa zamani, nimezidi kuwa na akili yenye kupambanua mabaya na mazuri na kuchukua hatua ili kuenda na kasi ya ukuaji wa akili yangu. Namshukuru Mungu ananiongoza vyema na naona baraka anazonipatia.

Nimeingia katika migogoro ya hapa na pale kama kutukanana na watu kwenye mitandao na yote hayo ni aidha kwa kufahamu au kutofahamu lakini kwa kuwa yamepita basi niyaache tu na niendelee na safari ya maisha nikiwa mpya kabisa. Fanbase nayo haikuniacha ilikuwa na mimi wakati wote huo kama ugomvi basi walipigana kwa ajili yangu. 

Lakini pia inawezekana niliwahi kuwakwaza watu kwa mambo yangu, nichukue fursa hii KUWAOMBA SAMAHANI na kuwaahidi kuwa haitokuja kutokea tena kwa sababu Hamisa wa sasa nimebadilika na ndio maana sitahitaji tena kuingia kwenye ugomvi wa aina yoyote na mtu yeyote yule katika maisha yangu na pia niwaombe mashabiki zangu na Fanbase kwa ujumla iwe kwenye groups za whatsapp au pages za kwenye social media kutojihusisha na ugomvi au matusi na mtu yeyote atakaetaka ugomvi na mimi na badala yake nguvu kubwa iwe kwenye kuendelea kuni’support kwa nguvu kubwa. Nia yangu ni kutowaingiza wale wanaonipenda katika matatizo kwa sababu hawastahili hata kidogo kupata shida kwa sababu yangu. Ninawapenda mno

Namalizia kwa kurudia tena ‘Dunia inaenda mbele na watu wanabadilika’. #NewHamisa#NewLife

Part 2 . tu na niendelee na safari ya maisha nikiwa mpya kabisa. Fanbase nayo haikuniacha ilikuwa na mimi wakati wote huo kama ugomvi basi walipigana kwa ajili yangu. Lakini pia inawezekana niliwahi kuwakwaza watu kwa mambo yangu, nichukue fursa hii KUWAOMBA SAMAHANI na kuwaahidi kuwa haitokuja kutokea tena kwa sababu Hamisa wa sasa nimebadilika na ndio maana sitahitaji tena kuingia kwenye ugomvi wa aina yoyote na mtu yeyote yule katika maisha yangu na pia niwaombe mashabiki zangu na Fanbase kwa ujumla iwe kwenye groups za whatsapp au pages za kwenye social media kutojihusisha na ugomvi au matusi na mtu yeyote atakaetaka ugomvi na mimi na badala yake nguvu kubwa iwe kwenye kuendelea kuni’support kwa nguvu kubwa. Nia yangu ni kutowaingiza wale wanaonipenda katika matatizo kwa sababu hawastahili hata kidogo kupata shida kwa sababu yangu. Ninawapenda mno Namalizia kwa kurudia tena ‘Dunia inaenda mbele na watu wanabadilika’ #NewHamisa #NewLife Asante na barikiwa sana! #Balozi

A post shared by HamisaMobetto (@hamisamobetto) on

Leave a Reply

Your email address will not be published.



Don't Miss