mohaKiongozi anaye panga maasi huanza kwa kuzima sauti za wanyonge, watetezi wao na hata vyombo vya habari.
Hatua ya pili ni kuzidisha idadi ya polisi na pamoja vifaa vyao vya kivita. Kama ilivyo fanya serikali yetu. Hatua hii hupasha ujumbe mmoja – tuko tayari kushinda kwa vyovyote.
Ngoma hii hukamilishwa kupitia vinywa vya viongozi ghushi ambao kazi yao huwa ni kutoa matamshi ya kuwatishia wakenya. Utawasikia wakisema wazi wazi kuwa wataiba na hata kununua kura wakati wa uchaguzi mkuu ujao. Hivyo mwenye hekia huenda asitamaushwe na ile hatua ya kuwanyang’anya watu fulani bastola zao walizopewa baada ya kufuata utaratibu wote unaotakiwa na serikali. Hii ndio sura kamili ya serikali ya Jubilee ambao sasa wanajiita JAP. Katika maeneo ya pwani, JAP inajulikana kama jambazi aliyeingia Pwani.
Msemo huu ulibuniwa hivi majuzi wakati wa kampeni za CORD na Kanu kule Malindi na hata Kericho.Wakenya wameona yale yanayo mpata Gavana wa Mombasa ndugu Ali Hassan Joho. NIngependa kuchambua kisa hiki cha Joho kwa kuwarejelea  Nelson Marwa, Joseph Nkaissery na rais wetu Uhuru Kenyatta.
Rais Uhuru Kenyatta
Ameonekana kama Rais asiyeweza chenga wala kupiga kona katika dimba hili la uongozi. Amekuwa wembu butu kwa wakenya. Rais ambaye wengi wemshtumu kwa kufanya ziara chungu mzima, ameonekana kama kiongozi anayeogopa kutoa maamuzi ya busara kuendeleza taifa. Wengi walimshuku pale alipopasua mbarika na kusema wazi kuwa ufisadi umekita mizizi ofisini mwake lakini akashindwa kuchukua hataua. Hivyo wengi walisema rais alijigubika katika uongozi almuradi kujiondoa katika minyororo ya ICC — siyo uongozi wa taifa. Wengine wamemtaja kama rais wa burudani anaye penda mambo ya kisasa. Yeye ni kijana. Haya yote ni maoni ya baadhi ya wakenya. Rais Uhuru anafahamu fika yote yanayotendeka humu nchini.
Anajua masaibu yote yanayompata Ali Hassan Joho. Bila shaka anajua shida za taifa hili lakini anaonekana kutojali. Atajali vipi na hajachukua hatua za dharura kuwanyamazisha wafisadi? Asichojua rais ni kuwa Kenya imebadilika, si ya zamani tena. Kenya sio kama taifa za Uganda ama hata Burundi.
Wakenya ni wasomi na wenye ujanja. Siasa za mimi ndio jogoo zilipitwa na wakati. Dhulma, unyanyasaji na ufisadi zimewafika wa Kenya kooni tangu mwaka wa 2013.
Wanachojaribu kufanya sasa ni kupima maji pwani ya Kenya. Wakenya wasipofanya lolote basi wataendeleza sera hizo kwingine. Lakini mtafeli. Rais umefeli pakubwa, na iwapo hutachukua hatua za dharura basi utazidi kuwagawanya wakenya kwa misingi ya kikabila. Uhuru Kenyatta babako alipokuwa Rais hakuwasaidia wana-gatundu wala kabila lake. Wana-gatundu ni maskini wakubwa hadi wa leo lakini kwa sababu ya siasa za kikabila hawaoni lolote baya na hilo. Uhuru Kenyatta fungua macho na ukomboe taifa hili. Usikubali wanaokuzunguka kuendelea kuzalisha chuki miongoni mwa wakenya. Kenya itabadilika!
Joseph Nkaissery
Joseph Nkaissery leo hii unatumia nguvu za bunduki na hata matamshi yako kuwahadaa wakenya pamoja. Wakati ule ilikuwa mimi na mwandishi habari mwenzangu Yassin Juma. Leo ni Gavana wa Mombasa Ali Hassan Joho.
Polisi wako wamekuwa vipofu wasioona maasi yanayotekelezwa na serikali yako.
Mmeshindwa kuwakamata wezi wa mali ya umma na badala yake kuwahangaisha kina yahe. Mmeshindwa kuwashika wezi wa Eurobond, NYS, Chicken Gate miongoni mwa wezi wengine wanaovalia suti na kujifanya bora zaidi ya wakenya wengine. Joseph Nkaissery siasa si mchezo mchafu, uchafu ni mtu mwenyewe.Usiondoke na jina baya, rekebisha na uache kusikiza vitoto vidogo vya mtandao vinavyokupa ushauri wa chochoroni. Kesho utakuwa raia kama wakenya wengine, utadharauliwa kwa yale yote uliofanya ukiwa uongozini, utakuwa kama yatima na kila ukifungua kinywa utanyamazishwa kutokana na uongozi wako feki wa kuabudu miungu yako midogo. Ni mawaidha tu usije ukanuna na kunitumania wanajeshi!
Nelson Marwa
Leo sina la kukueleza maana hata sijui nianzie wapi. Jifungie chumbani na ujiulize maswali ya mambo unayoyafanya. Ukipata jawabu basi anza kujirekebisha.
SDE